Thursday, 21 January 2021

ALIYESHUKA KUJISAIDIA AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TRENI AKIDANDIA

...

Picha ya mfano wa treni
Na Mwandishi wetu  - Moshi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Noa amefariki dunia baada ya kukanyagwa na treni ya abiria akiidandia wakati ikiwa imeanza kuondoka katika stesheni ya Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Noa anayedaiwa kuwa fundi ujenzi na aliyekuwa akitoka Dar es Salaam kwenda Arusha amekanyagwa na treni wakati akijaribu kudandia treni hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Arusha leo Alhamis Januari 21,2021.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa treni hiyo ilipofika tesheni ya Moshi, Noa alishuka na kwenda kujisaidia na hivyo treni hiyo kumuacha na alipojaribu kuikimbiza ili apande kwenye behewa lake kwa bahati mbaya aliteleza na ikamkanyaga na kumkata vipande
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger