Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo ametangaza kuanzia Februari mosi hadi 7, 2021 zitakuwa siku saba za kupiga nyungu kwa Watanzania ili kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona.
Akizungumza mkoani Tabora leo Jumamosi Januari 30, 2021 katika ziara ya Rais John Magufuli, waziri huyo amesema wananchi wanatakiwa kuendelea na majukumu ya kujenga Taifa bila hofu sambamba na kuchukua tahadhari kwa kupiga nyungu akimaanisha kujifukiza.
"Hakuna Mtanzania atajifungia ndani kwa ajili ya hofu ya ugonjwa huu wote tutapiga nyungu kuanzia Februari moja mpaka saba baada ya hapo shughuli nyingine ziendelee kama kawaida,” amesema Waziri Jafo.
Amesema hakuna hofu ya kuacha kufanya shughuli za maendeleo na nyungu ni shughuli inayotakiwa kufanyika mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment