Mchungaji mmoja kutoka eneo la Nkpor, Idemili Kaskazini lililopo katika jimbo la Anambra nchini Nigeria, kwa jina Onye Eze Jesus, ameomba msamaha kwa umma kwa video yake ya utupu iliyosambaa sana mitandaoni ambapo alionekana akiwadondoshea fedhaa baadhi ya waumini wa kanisa lake huku akiwaombea wakati hajavaa nguo wakiwa katika mto.
Onye Eze Jesus ameomba radhi kwa kupeperusha fedha namna ile pamoja na kuonesha watu wakiwa hawajavaa nguo katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa hatorudia tena.
"Ninawaomba radhi raia wa Nigeria na kila mtu kwa kosa la kupeperusha fedha kwa namna ile pamoja na kuwaonesha watu wakiwa hawana nguo katika mitandao ya kijamii.
Ilienda mtandaoni kimakosa na haitajirudia tena. Kuna watu wanaweka taarifa katika kurasa yangu na nilipogundua nilifuta haraka lakini kumbe baadhi ya watu tayari walikuwa wameishirikisha kwa wengine."
Mchungaji huyu ameomba radhi mara baada ya mamlaka ya jimbo la Anambra, ambayo imetoa onyo kali dhidi ya kutumia dini katika mambo yasiyo na maadili.
Onye Eze ni mchungaji wa jimbo la Anambra
Kamishina wa jimbo la Anambra ,Don Adinuba alisema alipata madai kuwa mchungaji huyo alikuwa anasaidia watu kuinua uchumi wao kwa njia za miujiza.
Wafuasi wake huwa wanamwagiwa fedha mara kwa mara kwenye mto na wafuasi hao kuoga mtoni wakiwa hawana nguo.
Suala la kuwaweka katika mitandao ya kijamii
Kwa waumini hao kuonekana mtandaoni ni jambo la aibu kwa jimbo hilo kwa ujumla, watu wa Anambra wanajulikana duniani kuwa ni watu wenye kupenda kufanya kazi.
"Onyeze Jesus anahamasisha mambo ya kishirikina, kusadikika na imani za potofu ambazo si nzuri katika jamii; ndugu zangu, marafiki na wafanyabiashara hizi nguvu za giza zinatupeka kubaya.
Masuala ya kishirikina kama haya yanaweza kuleta uadui bila sababu ya msingi na watu wanaweza kugombana hata kuuana bila sababu ya msingi.
Nimelazimika kukemea tabia hii na kuchukua hatua dhidi ya watu wazima waliopiga picha wakiwa hawana nguo na waliosambaza video hiyo,
Mchungaji Onyeze Jesus yuko hatiani kwa kuwanyima wafuasi wake haki ya kulinda utu wao na kukiuka sheria ya Nigeria kwa kuhamasisha mambo ambayo yapo kinyume na maadili."
Mchungaji huyo alikuwa anawahidi wafuasi wake kuwa wanaweza kuwa mamilionea kwa usiku mmoja tu na kutokana na mambo kama hayo serikali itachukua hatua madhubuti.
Onye Eze Jesus aliomba radhi na kuelezea kuwa anafanya kazi tofauti na wachungaji wengine lakini vilevile aliomba radhi kwa kumwaga fedha kwa namna ile.
Aliongeza kusema kuwa tayari video hiyo ameifuta katika kurasa yake ingawa tayari imeshirikishwa na watu wengi.
Chanzo - BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment