Mwendesha baiskeli wa kike aliongeza ladha kwenye mtindo wa hafla ya harusi baada ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake katika sherehe iliyotawaliwa na baiskeli.
Kulingana na Sierraloaded, mrembo huyo mwenye bidii alifunga pingu za maisha na mpenzi wake siku ya wikendi akiwa amebebwa na baiskeli.
Kawaida hafla za harusi hutawaliwa na magari, na wakati mwingine farasi lakini baiskeli ni tajira hadhimu.
Harusi hiyo ambayo iliandaliwa Makeni nchini Sierra Leone, ilihudhuriwa na waendeshaji baskeli ambao walijitokeza kushereheaka pamoja na mrembo huyo ambaye ameweka rekodi kwenye nyanja hiyo nchini Sierra Leone.
Kando na kuwa fundi wa baiskeli, Isata Sama Mondeh pia ni mwendesha baiskeli wa kwanza wa kike kujitosa kwenye biashara hiyo ambapo amewaajiri waendeshaji kadhaa kumfanyia kazi.
Isata, ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Tour de Lunsar ambapo alinyakuwa ushindi anapenda kuwatia moyo na kuwashauri wasichana wadogo, familia na jamii kuhusu masuala ya tamaduni. Ushauri wake utamfaa kila mwanamke ambaye anatazamia kuingia kwenye tasisi ya ndoa kwani si lazima utumie magari kwenye harusi ndio uhisi kuoleka.
0 comments:
Post a Comment