Monday, 2 November 2020

WANAFUNZI WANNE WAFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI NA AFISA ARDHI NYANG'WALE

...
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Hanry Mwaibambe

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Afisa ardhi wilaya ya Nyangwale Agustino Sibeye kwa kuwagonga na gari wanafunzi wanne wa shule ya msingi Ibambilwa na kufariki dunia wakati wakivuka barabara kuelekea shuleni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Hanry Mwaibambe amesema afisa huyo wa ardhi aliyejulikana kwa jina la Agustino Sibeye alisababisha vifo hivyo akiwa kwenye mwendo kasi eneo la makazi ya watu bila kuchukua tahadhari.

Wakati huo huo jeshi hilo linamshikilia Vestina Michael mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Mariamu Msalaba wakati akimtoa mimba nyumbani kwake kama anavyobainisha kamanda huyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger