Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) limeainisha mchango wa taaluma ya Jiolojia katika utekelezaji wa Miradi yake, kuanzia hatua za awali za utafiti na katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme.
Akizungumza katika kikao kazi cha Wajiolojia kinachoendelea katika ukumbi wa Benki Kuu, Jijini Mwanza, Mhandisi Eliaza Wangwe, ambaye ni Mjiolojia katika mradi wa Kufua Umeme wa JNHPP, amesema TANESCO ni miongoni mwa Taasisi zinazo watumia Wajiolojia katika tafiti zake za udongo na miamba katika ujenzi wa Miradi mbalimbali.
"Kikao kazi hiki ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kuelimisha wataalamu wa miamba na udongo jinsi gani TANESCO inawatumia katika ujenzi wa miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere wa MW 2115" amesema Mhandisi Wangwe.
Aidha, aliongezea kuwa ujenzi wowote kabla haujafanyika nilazima watalaamu wa miamba wakague na kujua aina ya miamba na udogo kwenye eneo husika ili kuwezesha usanifu wa msingi (foundation design).
Wataalamu hao wa miamba (wajiolojia) kutoka taasisi na Mashirika mbalimbali walipata fursa ya kupata elimu kuhusu masuala ya umeme katika banda la TANESCO.
Aidha, Wajiolojia wamewapongeza TANESCO, kwa kuweza kuwatumia wataalamu hao kwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake.
Lengo la kikao kazi hicho kilichoanza Novemba 25, 2020 ni kufanya tathimini ya mwaka katika shughuli zinazofanywa na watalaamu wa tasinia muhimu ya Miamba na Udongo inchini alisema Mwenyekiti wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS) Pro. Abdulkarim Mruma
0 comments:
Post a Comment