Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.
Na Josephat Lazaro - Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amefika na kuzungumza na Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.
Katika ziara hiyo Mh. Mbunge amepokea taarifa ya Maendeleo ya Miradi hiyo na kuongea na watendaji wa DAWASA.
Akizungumza Meneja wa Dawasa Chalinze, Onest Makoi alieleza kuwa Miradi yote inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka 2021 na wananchi wawe tayari kwa maboresho hayo yakiwemo upanuzi wa miundombinu ya Maji, umaliziaji wa Ujenzi wa Matenki na usambazaji awamu ya Tatu.
Pia , Alieleza kuhusu ujenzi wa mradi wa Ruvu-Mboga ambapo Ununuzi wa Vifaa kwa ajili ya ujenzi uko hatua ya Mwisho.
Kwa upande wa Mh. Mbunge aliwashukuru DAWASA kwa hatua kubwa wanazoendelea kufanya na kumshukuru Mheshimiwa Raisi kwa kuendelea kuwaangalia wananchi wanyonge wa Chalinze kwa kuendelea kutatua kero mbalimbali ikiwemo za Maji.
Ziara ya Kutembelea sehemu za huduma za Jamii zinaendelea na leo anaendelea kwa kutembelea Ofisi za TARURA kujua hali ya maandalizi ya marekebisho ya Miundombinu ya barabara vijijini na mijini.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa katika ofisi ya Meneja DAWASA-Chalinze, Bw. Onest Makoi wakati wa ziara maalum alipotembelea miradi ya Maji inayoendelea jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa maafisa wa DAWASA Chalinze kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.
0 comments:
Post a Comment