Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.
Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.
Aidha RC Kunenge amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.
Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.
0 comments:
Post a Comment