Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa siku mbili kwa wanachama wake 19, ambao jana walikula viapo Bungeni vya kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachofanyika Novemba 27, 2020.
"Kwa kuwa jambo hili ni la dharura natangaza wito (Public notice), kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana, kufika makao makuu ya chama bila kukosa siku ya Ijumaaa ya Novemba 27, 2020, saa 2:00 asubuhi, kutoka popote pale walipo kamati kuu inaweza kuchukua hatua za dharura kama itaona maslahi ya jumla ya chama yanaweza kuathiriwa", amesema John Mnyika.
Aidha Mnyika akizungumzia suala la wabunge hao kula kiapo hicho amesema kuwa, "Mimi kama Katibu Mkuu hakuna fomu yoyote ya mtu yeyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yeyote, hii fomu pia ina sehemu ya kujazwa na kiapo cha hakimu kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi ni kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi, wameenda kuapishwa bila baraka ya chama".
Wabunge 19 wanaotakiwa kuwasili siku ya ijumaa ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko na wengine walioapishwa kwa siku ya jana katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment