Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) imemkamata Rwegasira Samson kijiji cha Kinang’weli, Itimila Mkoani Simiyu
Rwegasira alijificha baada ya TAKUKURU kutangaza kuwa inamtafuta ili kumjumuisha kwenye kesi ya Uhujumu Uchumi namba ECC 87/2020 iliyokuwa na washtakiwa wengine watatu
Kesi hiyo inahusu makosa ya Rushwa, Ubadhirifu, Utakatishaji fedha na Ukwepaji kodi unaohusisha zaidi ya Tsh Bilioni 1.6
Rwegasira alikuwa ni Meneja wa Fedha wa Kampuni ya BEVCO limited inayojihusisha na uagizaji na uuzaji wa vinywaji vikali kutoka nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment