Friday, 6 November 2020

Waangalizi wa Kimataifa: Madai ya Trump Hayana Msingi

...


Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi wa Marekani amesema jana kwamba madai ya Rais Donald Trump hayana msingi, yanayosema kwamba kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi huo.

Michael Georg Link anayeongoza ujumbe wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) ameongeza kuwa madai ya Trump yanadhoofisha imani ya umma kwa taasisi za kidemokrasia nchini humo.

Katika ripoti ya awali, ujumbe huo pia ulionya kwamba matamshi ya Trump wakati wa kampeni zake, yaliangaliwa na wengi kuwa na uwezo wa kuchochea vurugu za kisiasa baada ya uchaguzi.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger