Saturday, 21 November 2020

TBS NA ZBS WAANDAA TUZO YA UBORA YA SADC KWA WAFANYABIASHARA NA WAZALISHAJI WA BIDHAA

...

  

Afisa Viwango Mkuu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Nickonia Mwabuka akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam


Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa nchini wametakiwa kushiriki katika shindano la utoaji tuzo bora kwa makampuni ya uzalishaji na watoa huduma itakayofanyika Machi mwaka 2021 nchini Msumbiji katika mkutano wa mwaka unaoshughulikia vikwazo katika biashara kwenye Jumuiya ya SADC (SADCTBT-Cooperation Structures).

Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango Mkuu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Nickonia Mwabuka amesema tuzo hizo ni kuangalia bidhaa zetu zinakidhi ubora katika utengenezaji na utumiaji kwaajili ya wananchi na biashara pamoja na kukuza uchumi kwa jumuiya ya SADC.

"Tunawaomba wadau wote katika uzalishaji na kutoa huduma kutumia nafasi hii ya kushindana iliyotolewa na SADC, kujaza fomu husika kwa kuangalia vigezo vilivyowekwa na kutuma TBS kwa mtandao uliowekwa, kama upo karibu unaweza kuleta mwisho ni Jumatano saa 10 jioni".Amesema Bw.Mwabuka.

Aidha Bw.Mwabuka amesema makundi yote yatakayo shiriki watajaza fomu maalumu iliyoandaliwa ambayo ipo kwenye tovuti ya TBS- www.tbs.go.tz, ZBS- www.zbs.go.tz na kuirejesha kwa kutumia email qualityawards@tbs.go.tz Novemba 25 mwaka huu.

Pamoja na hayo Bw.Mwabuka amesema mshindi wa kwanza katika kila kundi atapewa cheti cha ushindani na kombe.

"Washindi hao pia watashiriki katika mkutano wa SADCTBT utakaofanyika Machi 2021 Maputo nchini Msumbiji ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa SADC". Amesema Bw.Mwabuka.

Hata hivyo amesema kuwa faida ya kushiriki katika mashindano hayo ni pamoja na kufanya bidhaa na huduma zetu kwa ujumla kujulikana katika soko la SADC.

Sambamba na hayo amesema kuwa makundi ambayo yatashiriki ambayo ni kundi la wajasiriamali chini ya watu 100,Wazalishaji wakati ma wakubwa zaidi ya wafanyakazi 100,mtu binafsi anayezalisha/kutoa huduma inayokidhi ubora.

Amesema utoaji wa tuzo kwa makampuni ya uzalishaji na watoa huduma ni utaratibu ambao hufanyika kila mwaka kwa wanachama wa SADC kwa lengo la kutambua mchango wa matumizi ya viwango katika kukidhi ubora wa bidhaa na huduma kwa jamii ya SADC.

Tuzo ya hizo zimeandaliwa na Shirika la Viwango TBS na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) wakishirikiana na taasisi za sekta binafsi bara na visiwani.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger