Friday, 13 November 2020

SERIKALI KUNUNUA NDEGE YA MIZIGO..... KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) CHAHAMISHIWA OFISI YA RAIS

...


 Rais  Magufuli amesema kipindi cha miaka mitano ijayo serikali yake imepanga kuendeleza miundo mbinu kwa kununua ndege moja ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya bustani, minofu ya samaki na nyama lengo ni kuwafanya wakulima watajirike kutokana na kazi wanayofanya.

Rais Dk Magufuli ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 12 huku akilihutubia  bunge hilo na Taifa kwa ujumla na kusema  kuwa lengo lake ni kuona kila mtanzania ananufaika na maendeleo ya ukuaji uchumi nchini.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake imepanga kuongeza tija kwenye kilimo kwa kukifanya kuwa cha kibiashara lengo likiwa kuwa na hifadhi kubwa ya chakula, malighafi za viwandani na kuuza pia nje ya nchi hivyo upatikanaji wa mbegu na zana za kilimo zitaboreshwa.


Pia Dkt.Magufuli  amekihamisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ofisi ya Rais.Amesema kuwa anataka kupambana na wale wanaokwamisha uwekezaji, kwani anataka muwekezaji apewe kibali ndani ya siku 14.


“Nataka muwekezaji mwenye fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14, na kwa sababu hiyo nimeamua suala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na Kituo Cha Uwekezaji  (TIC) kulihamishia kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda ofisi ya Rais, ili wanaokwamisha nikapambane nao mwenyewe”.amesema Rais Magufuli




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger