Thursday, 19 November 2020

RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU SARUJI KUUZWA BEI JUU

...

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua bei ya Saruji kwenye moja ya ghara mjini Shinyanga.
****

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amebaini sababu za wafanyabiashara kupandisha bei ya Saruji mkoani humo, na kupiga marufu kuuza bei ya juu.

Mfuko wa Saruji mkoani humo una oanzia pointi 32 na 42, unauzwa kwa bei moja kuanzia shilingi 20,000/= ,21,000/= hadi 22,000/=, kwa wafanyabiashara wa maduka, lakini wenye maghara wanauza tofauti mfuko wa pointi 32 ni Shilingi 17,500/=, na 42 ni 18,000/=.

Telack alibaini utofauti huo  jana alipofanya ziara ya kukagua bei ya Saruji kwenye maduka na maghara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga, na kusema kuwa Saruji ipo ya kutosha, isipokuwa kuna ujanja ambao unafanyika kwa wafanyabishara kutaka faida kubwa.

"Nimebaini kuna ujanja ambao unafanyika wa kuuza Saruji, wafanyabiashara wa kawaida wananunua Saruji kwa wenye maghara bei ya kawaida shilingi 17,500/= na 18,000/=, lakini wao wanapandishia wananchi na kuuza zaidi ya 20,000/=," alisema Telack.

"Kuanzia sasa napiga marufuku kwa wafanyabiashara, hakuna kuuzia wananchi bei ya saruji kuanzia shilingi 20,000/= bali bei iwechini ,waache kutaka kupata faida kubwa na kuumiza wananchi," aliongeza.

Naye mmoja wa wafanyabiashara wa kuuza Saruji kwenye maduka John Ngalya, alikiri kupandisha bei ya saruji, kwa madai kuwa na wao wanauziwa bei ya juu kutoka kwa wanunuzi wakubwa wanaotoa Saruji moja kwa moja kutoka viwandani.

Kwa upande wake wakala wa kusambaza Saruji kwa wafanyabiashara kutoka  viwandani Shufaa Mabula, alisema bei ya Saruji imepanda kutokana na uzalishaji kuwa mdogo tena wa older, na kusababisha kuingia gharama ya kusubili mzigo.

Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Estormine Henry, waliipongeza Serikali kuingilia kati suala hilo la kupanda kwa Saruji ambalo lilisababisha kupanda kwa gharama za ujenzi.
Zoezi la ukaguzi bei ya Saruji likiendelea.
Mmoja wa mawakala wa usambazaji saruji kutoka viwandani Shufaa Mabula (kushoto),akielezea sababu za kupanda kwa bei ya Saruji, kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger