Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema utumbuaji kwa watumishi wa umma wazembe, wala rushwa, wezi na wabadhirifu, utaendelea katika miaka mitano ijayo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema, watumishi wezi, wabadhirifu bado wapo hivyo ataendelea kuwang’oa.
“Watumishi wazembe, wala rushwa, wezi, wala mali bado wapo. Miaka mitano ijayo tutawashughulikia, kwa kifupi niseme utumbuaji utaendelea,” amesema Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment