Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema lengo la demokrasia sio kusababisha vurugu na kwamba hakuna demokrasia isiyo na mipaka.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020, Rais Magufuli amesema, uhuru na haki vinakwenda sambamba na wajibu.
“Katika miaka mitano tutaendelea kukuza demokrasia, kulinda uhuru na haki ya wananchi na vyombo vya habari. Hata hivyo, ningependa kukumbusha kuwa lengo la demokrasia ni kuleta maendeleo na siyo fujo na hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka”.
“Uhuru na haki vinakwenda sambamban na wajibu na hakuna uhuru na wajibu usiokuwa na haki vyote vinakwenda sambamba na najua nimeeleweka vizuri,” amesema Rais John Magufuli.
Via Mwanahalisi Online
0 comments:
Post a Comment