Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya vurugu mkoani kwake na kueleza kuwa sheria itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani.
Kunenge ametoa onyo hilo wakati wa Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa jiji lipo kwenye hali ya amani na utulivu huku usalama ukiwa umeimarishwa.
0 comments:
Post a Comment