Tuesday, 3 November 2020

Mbunge wa mteule wa CHADEMA asema hatowasaliti wananchi waliomchagua

...


Aida Khenan, Mbunge Mteule wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA amesema, hatowasaliti wananchi waliomchagua hivyo atakwenda Bunge kuapishwa ili aweze kuwatumikia.

Aida ni Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CHADEMA aliyetangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, akimshinda Ally Kessy wa CCM aliyekuwa anatetea jimbo hilo aliloongoza kwa miaka 10.

Kauli hiyo imekuja baada CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kutoyatambua matokeo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hata kwenye maeneo waliyoshinda.

Katika Bunge lililopita, Aida alikuwa Mbunge wa Viti Maalum. Lakini sasa amesema yeye ni Mbunge ambaye anasubiri kuapishwa
.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger