Mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden ameendelea kupata kura zaidi katika majimbo yenye ushindani mkali hasa Georgia na Pennsylvania. Hayo yakijiri, Rais Donald Trump amedai wizi wa kura unafanywa dhidi yake.
Kulingana na kura maalum zinazobaini nani mshindi wa urais, yaani 'electoral votes' kwa Kiingereza, Biden anazo jumla ya kura 253 huku Rais Donald Trump akiwa na kura 214. Hayo ni kulingana na baadhi ya vituo vya televisheni nchini humo.
Lakini kulingana na shirika la habari la Associated Press pamoja na Kituo cha Fox News, Biden anaongoza kwa jumla ya kura 264, ikiwa wamejumuisha pia kura kutoka jimbo la Arizona. Mshindi anahitajika kupata kura maalum zisizopungua 270.
Joe Biden aliye na umri wa miaka 77 na ambaye pia ni makamu wa zamani wa rais huenda akawa rais mpya ikiwa atashinda kura katika jimbo la Pennsylvania au kwa kushinda majimbo mawili kati ya Georgia, Nevada na Arizona.
Nafasi ya Rais Trump kushinda inaonekana kuendelea kuwa ndogo, kwani anahitajika kupata ushindi kwenye majimbo ya Pennsylvania na Georgia na pia ampiku Biden katika majimbo ya Nevada na Arizona.
0 comments:
Post a Comment