Monday, 2 November 2020

INFINIX Yaendelea Kutamba Sokoni.......Kaa Tayari Kushuhudia Mp64 Za Kamera Ya Note 8 Zinavyofanya Kazi

...

Kama ni NOTE basi si nyengine hiyo ni Infinix NOTE 8 ndio mdahalo uliopo sasa kwenye page ya Infinix XClub Tanzania ‘http://www.infinix.club’. 


Kampuni ya Infinix imekuwa ikiaminika kwa mapinduzi wanayoendelea kuyafanya katika soko la simu na hivi punde kupitia picha zilizovuja katika mitandao ya kijamii inasemakana Infinix imejipanga kuendeleza mapinduzi hayo kwa ujio wa toleo la NOTE. 


Toleo hilo jipya linalosemekana ni Infinix NOTE 8 inasemekana huwenda ikawa simu kali zaidi kwa mwaka huu wa 2020 kutoka na processor yake aina ya Helio G80 kuwa moja ya processor zenye kasi ya ajabu zaidi ya processor yoyote kutokea kwa mwaka huu wa 2020 alisema Bwana Masawe Simba mdau wa simu za Infinix.

Baada ya tetesi hizi sikusita kumvutia waya Aisha Karupa Afisa wa Mahusiano wa Infinix na alikiri kuhusu ujio wa simu aina ya NOTE 8 na kudai ni kweli ni "simu yenye processor kubwa Helio G80 kwa kifupi si simu ya kulinganisha na toleo lolote la awali la Infinix lakini pia uzinduzi wake ni wakipekee haujawai fanyika na Kampuni yoyote ya simu nchini Tanzania. 


Alisistiza tuweni na subra, tujichange NOTE 8 si processor tu kali kwani hata kamera ni kali zaidi shuhudia 64MP Ultra HD 6 za kamera ya NOTE 8 zinavyofanya kazi kwenye NOTE 8 safari hii tumecheza na teknolojia vilivyo” 


Baada ya kuambulia machache kuhusu Infinix NOTE 8 nikaona sio mbaya kuwajuza na nyinyi wadau wenzangu wa simu nzuri lakini je unaisi hii simu uzinduzi wake utakuwa wa aina gani?




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger