Bunge la Tanzania limemuidhinisha mbunge wa Ruangwa (CCM), Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu baada ya kupigiwa kura za ndiyo 350.
Uteuzi wa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu umefanywa na Rais John Magufuli leo Alhamisi Novemba 12, 2020 na jina lake kuwasilishwa bungeni na mpambe wa Rais.
Baada ya kuwasilishwa, Spika Job Ndugai aliwatangazia wabunge kuhusu uteuzi huo, kisha wawakilishi hao wa wananchi kupiga kura ya kumuidhinisha.
Katika ya kura 350 zilizopigwa, wabunge wote walipiga kura ya ndio kumuidhinisha Majaliwa kuwa mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali.
"Idadi ya kura zilizopigwa ni 350, hakuna kura yoyote iliyoharibika, kura ya hapana hakuna hata moja zote 350 zimemthibitisha Mhe.Kassim Majaliwa, kwa hiyo waheshimiwa wabunge Mhe, Kassim Majaliwa amethibitishwa na bunge hili kuwa Waziri Mkuu kamili".Spika Ndugai
0 comments:
Post a Comment