Na Alex Sonna,Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja leo tarehe 12 Novemba 2020 limemthibitisha Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha muhula wa pili wa serikali ya awamu ya tano.
Uthibitisho huo umejiri mara baada ya jumla ya wabunge 350 kupiga kura za ndio sawa na asilimia 100.
Kassim Majaliwa atahudumu katika nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
0 comments:
Post a Comment