BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA
KUCHELEWA
KWA TATHMINI YA VYETI NA ULINGANISHO WA TUZO ZINAZOTOLEWA NA “NCC
EDUCATION NA ASSOCIATION OF BUSINESS EXECUTIVES- ABE, UK”
Baraza la
Taifa la Elimu Ufundi (NACTE), linapenda kuujulisha umma kuwa
limechelewesha utoaji wa majibu ya maombi ya tathmini ya vyeti na
ulinganisho wa tuzo zinazotolewa na NCC Education, UK na Association of
Business Executives- ABE, UK kwa kushirikiana na Taasisi binafsi za
Elimu ya Ufundi hapa nchini. Hii ni kutokana na kufanya upya uchambuzi
wa maombi hayo baada ya kubaini kuwepo kwa dosari katika hatua
mbalimbali za utoaji wa mafunzo hayo kama vile sifa za udahili,
uendeshaji wa mafunzo, upimaji na vyeti.
Kulingana
na taratibu za Baraza, ni haki ya mwombaji wa huduma hiyo kupewa majibu
ndani ya siku 30 baada ya kukamilisha taratibu zote za kutuma maombi.
Baraza linatambua kuwa uamuzi wake wa kuchambua upya na tathmini ya
maombi yote yaliyotumwa umeleta usumbufu kwa waombaji. Hivyo linaomba
radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Baraza
litakamilisha kazi ya kuchambua na kutathmini vyeti na ulinganisho wa
tuzo hizo na kutoa majibu kwa waombaji wote kabla ya tarehe 30/04/2016.
Asanteni kwa ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA;
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
Tarehe 6/4/2016
0 comments:
Post a Comment