Katika
siku za hivi karibuni katika maeneo mbalimbali hapa nchini,
kumejitokeza makundi ya watu ama mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi
fulani kujipatia kipato kwa njia za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi
vijana kwamba watawapatia ajira katika taasisi hizo.
Makundi
haya ya kihalifu imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali,
hivyo, ni suala ambalo linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi
ili kukomesha vitendo hivyo.
Juhudi
za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili kuwatia
mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.
Aidha,
kufuatia kuibuka kwa vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata
matapeli wawili wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro
na Mbeya, uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.
Jeshi
la Polisi likishirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama,
kimsingi, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na Ulinzi na
Usalama imara.
Tutaendelea kupambana na makundi haya ya kihalifu na utapeli ili nchi yetu iendelee kuwa salama.
Tunawasihi
wananchi kufuatilia taarifa kwenye vyanzo sahihi juu ya jambo lolote
wanalotaka kulifanya ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na baadhi ya
watu kwa lengo la kujipatia vipato.
Aidha, wananchi watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama kuhusu tabia na mienendo yoyote wanayoitilia mashaka.
Jeshi
la Polisi na vyombo vingine vyote vya Ulinzi na Usalama viko imara,
makundi ya kiuhalifu na wahalifu wote wajue hawana pa kukimbilia,
watakamatwa.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
0 comments:
Post a Comment