Serikali inatarajiwa kuwasilisha miswada
mbalimbali ya sheria katika Mkutano wa Bunge la Bajeti utakaloanza
kesho mjini Dodoma ili ijadiliwe na kupitishwa na wabunge.
Miswada mingi ya sheria imekuwa
ikilalamikiwa na wadau, hata Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge
la 11 mwaka jana, alilalamikia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011.
Alisema kuwa sheria hiyo inatoa mianya kwa watumishi kuiba fedha za umma.
Katika mkutano huo, Bunge linatarajia
kujadili na kupitisha miswada miwili ambayo ni wa Sheria ya Matumizi wa
mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya jana alisema Serikali itawasilisha
pia bungeni miswada mingine ya sheria ijadiliwe na kupitishwa baada ya
kupitisha bajeti kukamilika.
Hata hivyo, alisema Bunge bado
halijapokea miswada itakayowasilishwa na Serikali zaidi ya hiyo miwili,
lakini kuanzia Juni 24 hadi 30 zimetengwa kwa ajili ya kujadili miswada
mingineyo.
Mwandumbya alisema pamoja na shughuli
hizo, jumla ya maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali bungeni na
kila Alhamisi yataulizwa Maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na
anatarajia kujibu jumla ya maswali 88.
“Baada
ya wabunge kujadili miswada itakayowasilishwa na Serikali, hoja ya
kuahirisha Bunge itatolewa Julai Mosi. Hapo Bunge litakuwa limemaliza
kazi yake ya kujadili bajeti za wizara zote katika mkutano huu,”alisema Mwandumbya.
0 comments:
Post a Comment