Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
limeibuka na kukanusha taarifa zinazoenezwa na baadhi ya wananchi juu ya
kuwepo kwa mgao wa umeme kutokana na kukatika kwa umeme kunakoendelea
hivi sasa.
Katika mahojiano maalum na mtembezi.com
Kaimu Afisa Mahusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, amesema kukatika kwa
umeme kunasababishwa na uboreshaji wa miundombinu chakavu iliyodumu kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 20 na ujenzi wa vituo vipya vya umeme
vitakavyofanyakazi kwa ufanisi zaidi.
Aidha amewataka wananchi kuwa wavumilivu
kwa kipindi hiki cha maboresho yanayoendelea kufanyika na kuahidi mara
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo watapata umeme wa uhakika na
usiokatika mara kwa mara.
Ametoa wito kwa wananchi kushirikiana
kwa karibu na shirika hilo hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kuweza
kutatua kwa haraka changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment