Mtu
mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu
wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani
Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni
Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa
kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.
Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.
Kamugisha
alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu
na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia
alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti
2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa
kimapenzi.
Aliyejeruhiwa
katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo
aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia
wakati wakipigana.
Kamugisha
alisema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa
matibabu zaidi na kwamba, hali yake siyo nzuri.
Alisema
mke wa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi baada ya
mtuhumiwa na mmiliki wa kilabu hiyo kukimbia kusikojulikana.
Kamanda huyo alisema jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watu hao ili kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
0 comments:
Post a Comment