Sunday, 3 April 2016

Mtu mmoja auawa kikatili na kutelekezwa porini mkoani Morogoro

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wananchi wa kijiji cha Dete kata ya Tununguo wilaya ya Morogoro wamemtaka mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Stephene Kebwe kufika kijijini hapo kujionea utendaji kazi wa askari polisi wa kituo cha Ngerengere kufuatia mtu mmoja kuuawa kikatili na watu wasiojulikana bila askari wa kituo hicho kutoa msaada wowote kwa wananchi.

Wakizungumza kwa jazba wakati wa kuondoa mwili wa marehemu Abas Mwarabu aliyekutwa porini akiwa amefariki na kubaki fuvu na mifupa kutoka na kuchukua muda mrefu tangu alipo uawa wananchi hao wamesema endapo askari wa kituo hicho hawataondolewa wataandamana hadi kwa mkuu wa wilaya kupinga utendaji kazi wa askari wa kituo hicho.

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho Fabiani Bayo akizungumzia tukio hilo amesema huenda mauaji hayo yametokana na ugomvi wa kimapenzi kwani alisha pelekewa kesi hiyo na kabla hawaja zungumza ndipo mauaji hayo yakajitokeza huku ndugu wa marehemu Ramadhani Rashidi akieleza masikitiko yao juu ya kukosa msaada wa jeshi la polisi katika kuutafuta mwili wa marehemu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrch Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema watu watatu wanashikiliwa na jeshi hilo akiwemo Juma Evanda ambaye ndie aliye husika kumuita marehemu nyumbani kwake wakati wa uhai wake huku akiwataka wananchi kuwasiliana naye moja kwa moja wanapo ona askari hawawatendei haki wanapo peleka malalamiko na tarifa zinazo hitaji msaada wa polisi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger