Al-Douri
Runinga
nchini Iraq imeripoti kuwa Izzat Ibrahim
al-Douri, ambaye wakati mmoja
alikuwa makamu wa Rais Saddam Hussein na mmoja wawaanzilishi wa kundi la
Islamic State nchini Iraq, ameuawa.
BBC bado
haijapata taarifa rasmi ya kuthibitisha kifo chake, lakini picha na
maelezo kuhusu kifo cha Bwana Al Douri imeripotiwa pakubwa.
Iwapo taarifa hiyo ni kweli, kifo chake kitakuwa hatua kubwa kwa serikali ya Iraq dhidi ya makundi ya Jihadi.
Al Douri
ambaye daima ana masharubu mekundu, alikuwa mfalme katika kilabu kwenye
kadi zilizotolewa ili kusaidia majeshi ya Marekani kutawambua wanachama
katika utawala wa Saddam Hussein, mnamo mwaka 2003.BBC
0 comments:
Post a Comment