Watoto wawili wamekufa huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya baada ya ukuta wa nyumba waliyokuwa wamelala kuwaangukia na kuwafunika kitandani kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha mkoani Tanga.
Wakizungumza
na Mpekuzi katika eneo la tukio lililopo barabara ya 18 jijijni Tanga
viongozi wa serikali na wale wa wananchi wa eneo hilo wamesema limetokea
jana majira ya saa 11 Alfajiri wakati mvua iliyoambatana na upepo
ikinyesha ndipo ukuta wa nyumba hiyo uliojengwa na mawe makubwa ya
baharini ulipodondoka na kusababisha madhara hayo.
Waliokufa
katika eneo hilo wametajwa kuwa ni Bakari Shabani mwanafunzi wa darasa
la kwanza shule ya msingi Ngamiani kati na Hassan Abdala mwenye umri wa
mwaka mmoja ambao walifariki papo hapo huku wengine wawili wakijeruhiwa
vibaya akiwemo mama mzazi wa marehemu ambao wamelazwa katika hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
Kufuatia
hatua hiyo diwani Mbaruk ameiomba halmashauri ya jijij la Tanga pamoja
na idara ya majengo kufanya ukaguzi wa majengo chakavu hasa katika
kipindi hiki cha mvua za masika ili baadhi ya familia ziweze kuhamishwa
na kutafutiwa mahali pa kujisitiri ili kuepuka maafa makubwa dhidi ya
wahusika
0 comments:
Post a Comment