Wednesday 29 April 2015

YANGA KUATWAZWA MABINGWA MEI 6

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

waziri Fenela Mukangara wa kwanza kushoto akiikagua
timu ya Real Madrid (wastaafu) walipokuja Tanzania kucheza mechi ya kirafikiWaziri wa Habari, Vijana Utamuduni na Michezo nchini Tanzania , Dr. Fennela Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania hapo Mei 6, 2015 baada ya kuisha kwa mchezo kati ya mabingwa wapya, Yanga na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC.
Mechi hiyo haitakuwa na athari yoyote kwa Yanga kwa kutia doa sherehe za ubingwa wao hata kama Azam itashinda, kwani tayari wana pointi 55,ambazo hakuna timu yoyote inayoweza kuzifikia.
Makabidhiano ya kombe hilo yatafanyika katika uwanja wa taifa wa Dar es Salaam mbele ya mashabiki wapatao 50,000.
Tayari sherehe hizo zimeanza katika matawi mbalimbali ya timu hiyo, ambayo mwakano itashiriki kombe la Washindi barani Afrika.

 KUANGALIA SELECTION KIDATO CHA TANO 2015 BONYEZA HAPO CHINI


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger