Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli (katikati) akizungumza jambo, kulia ni Mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA, Kurwijira Maregesi pamoja na Msimamizi wa Mahesabu na Utawala kutoka AUDITAX.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli (katikati) akizungumza jambo,
kulia ni Mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania kutoka BASATA, Kurwijira
Maregesi pamoja na Msimamizi wa Mahesabu na Utawala kutoka AUDITAX.
Wanahabari wakichukua tukio.
Wanahabari wakichukua tukio.
BARAZA lasanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na bia ya Kilimanjaro, leo imetangaza rasmi majina ya wateule (nominees) wa vinyang’anyiro 32 vya tuzo za muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli alisema kuwa akademy ilikaa mwisho wa wiki iliyopita na kufanya kazi ngumu na nzito ya kupitia mapendekezo ya umma na hatimaye kuteua kwa njia ya kupiga kura.
“Zoezi la kupata wateule lilidumu kwa zaidi ya saa 18 kudhihirisha umahiri na kujituma kwa kundi la akademi,” alisema Kikuli.
Mchakato wa akademi ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala AUDITAX International ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa huru na haki.
Tanzania itapewa nafasi kuanza kupiga kura kwa kutumia njia zile ili kuchagua mshindi kwa kila kipengele.
Kura zitaanza kupigwa tarehe 5 Mei 2015 hadi Juni 5 2015. Njia za kupiga kura ni kama zifuatazo. 1. Whatsapp: 0686 528 813 2. SMS: 15415 3. Mtandao: www.ktma.co.tz
KUANGALIA SELECTION KIDATO CHA TANO 2015 BONYEZA HAPO CHINI
0 comments:
Post a Comment