MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema
hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga
na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kauli
ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo
tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya
viongozi wa umoja huo.
Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na MTANZANIA.
Mbowe
alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa
atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Hatuwezi
kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu
Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM,” alisema Mbowe.
Aprili
15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency
(ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama
vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa
mfumo unaowanyonya wananchi.
Zitto
alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama
vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani
0 comments:
Post a Comment