WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (pichani) ametoa tamko
kuhusiana na Watanzania waliopo nchini Afrika Kusini.
Waziri Membe amesema Watanzania 21 watarejeshwa nchini kutokana na vurugu zinazoendelea za wenyeji kuwashambulia wageni huko Afrika Kusini.
Aidha, Membe ameongeza kuwa Watanzania watatu wamefariki kwa maradhi lakini si kuuawa katika vurugu hizo, hivyo hakuna mtu aliyeuawa kutokana na machafuko yanayoendelea.
0 comments:
Post a Comment