MATUMAINI
ya Simba SC
kurudi kwenye michuano ya Afrika mwakani, jana yameanza
kuyeyuka baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Matokeo
hayo, yanaifanya Simba SC ibaki na pointi zake 35 baada ya kucheza mechi
22, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 42 za mechi 22. Yanga
SC wapo kileleni kwa pointi zao 46, baada ya kucheza mechi 21.
Mbeya
City ilipata bao lake la kwanza dakika za majeruhi kipindi cha kwanza,
mfungaji Paul Nonga aliyemalizia pasi ya Deus Kaseke iliyompita beki
Mganda, Juuko Murusheed. Mbeya City wameifunga Simba SC mabao 2-0 Sokoine jana
Katika mchezo huo, Simba SC ilipata pigo dakika ya 23, baada ya beki
wake tegemeo, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na
Mganda, Joseph Owino. Isihaka, beki anayeinukia vizuri aliumia baada ya kugongana na Peter Mapunda.
Mbeya
City ilipata bao lake pili dakika ya 69, mfungaji Peter Mwalyanzi,
aliyemalizia krosi Nonga aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Simba
jana.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa:
Hannington
Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Christian Sembuli, Juma
Nyoso, Kenny Ally, Peter Mapunda/Hassan Kibopile dk77, Raphael Daud,
Paul Nonga, Cossmas Freddy/Peter Mwalyanzi dk59 na Deus Kaseke.
Simba SC:
Peter
Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Juuko
Murusheed, Hassan Isihaka/Joseph Owino dk23, Abdi Banda, Jonas Mkude,
Elias Maguli/Issa Abdallah dk56, Ibrahim Hajibu, Said Ndemla na
Ramadhani Singano ‘Messi’.
0 comments:
Post a Comment