Takwimu
zilizotolewa na maafisa wa mchezo
wa kiungwana wa FA zinaeleza kuwa
Chelsea ni timu inayoongoza kutoheshimu maamuzi ya waamuzi katika ligi
kuu England, huku makocha wa timu hiyo wakishika nafasi ya pili kwa
utovu wa nidhamu wakati wa mechi.
Liverpool
imetajwa kuwa klabu yenye heshimu kubwa kwa waamuzi katika kipengele
hicho kilichobeba alama saba ikifuatiwa na Burnley na West Brom.
Klabu za
Arsenal na Stoke City zipo katikati katika orodha hiyo ambapo kanuni
zinaeleza kuwa kitendo cha kuheshimu maamuzi yenye utata bila kugoma au
kumzonga muamuzi kinaipa timu alama saba wakati tabia ya kukubali
maamuzi halafu kuonesha ishara za kutoheshimu zinatolewa alama sita.
FA
wanatoa alama kwa kuangalia maeneo sita ambayo ni kadi nyekundu na
njano, mchezo mzuri, heshima kwa wapinzani, heshima kwa waamuzi, tabia
ya maafisa wa timu na mashabiki.
Alama kumi zinatolewa kwa kadi nyekundu ambapo timu inapunguziwa alama moja kwa kadi ya njano na alama tatu kwa kadi nyekundu.
Mchezo
mzuri una alama kumi zinazotolewa kwa kucheza soka la kuvutia,
kushambulia sana na kushinda, lakini timu ikitumia mbinu za kujilinda na
udanganyifu alama zinapunguzwa.
Alama
saba zinatolewa katika kipengele cha heshima kwa wapinzani
kinachohusisha kuwaheshimu wachezaji pinzani na kuonesha mchezo wa
kiungwana, wakati alama saba pia zinatolewa kwa kuheshimu waamuzi na
maafisa wa mechi.
Alama
sita zinatolewa kwa maafisa wa timu wakiwemo makocha dhidi ya waamuzi,
wakati alama kumi zinatolewa kwa tabia ya mashabiki ambapo alama zote
zinatolewa kwa mashabiki wanaokubali matokeo, wakati wakitumia lugha ya
matusi kwa wachezaji, waamuzi na kuwatishia mashabiki pinzani alama
zinapounguzwa.
Chanzo:Shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment