Sunday 9 January 2022

WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI LA MTOTO, WATUPA MWILI WAKE MTAANI TANGA

...

Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya mara ya pili ya mtoto Sharifa Abasi ambaye mwili wake ulifukuliwa na watu wasiojulikana na kukutwa umetupwa mtaani. Mwili huo umezikwa tena leo katika kata ya Msasa wilayani Handeni mkoani Tanga. Picha na Rajabu Athumani.
 
***
Siku moja baada ya mwili wa mtoto Sharifa Abasi kuzikwa, kaburi lake limefukuliwa na watu wasiojulikana huku mwili wake ukikutwa umetupwa mtaani ukiwa bado ndani ya sanda.

Mwili huo wa mtoto ambaye aliyefariki akiwa na mwezi mmoja na wiki mbili ulizikwa jana Jumamosi Januari 8, 2022 umekutwa katika mtaa wa Msasa Shule wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akisimulia mkasa huo baba mkubwa wa marehemu, Athumani Ligotwe wakati wa mazishi ya pili ya mtoto huyo yaliyofanyika leo Jumapili asubuhi amesema ameshangazwa na tukio hilo kwani yeye ndio aliweka mwili wa marehemu kaburini jana na leo wamekuta kaburi limefukuliwa na mwili haupo.

Amesema alifika kwenye kaburi na kubaini mwili haupo na kurudi sehemu ambayo umeonekana na kuthibitisha kuwa ulikuwa wa mtoto wa mdogo wake ambaye alizikwa jana.

Hili ni tukio la kinyama sana lililotokea kwenye familia yetu, wamefukua kaburi ya mtoto wetu na kwenda kutupa mwili mita 300 kutoka hapa kwenye nyumba ya mtu, tunaomba Jeshi la Polisi kuwatafuta hawa watu", amesema Athumani

Chanzo - Mwananchi
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger