NCHI ya Norway imesema inajiandaa kuanza majaribio ya mabasi ya abiria (ya umma) ambayo hayana dereva, kuanzia mweiz Aprili, mwaka huu.
Mabasi hayo ya umeme ambayo yametengenezwa na Kampuni ya nchini Uturuki ya Karsan yana uwezo wa kubeba abiria 50 na yana urefu wa mita 8, siti 21 na eneo kubwa la watu kusimama na kwa sasa yameanza majaribio katika eneo la Forus Business Park kabla ya maeneo mengine.
Wakati wa majaribio kutakuwa na madereva kwenye magari hayo kwa ajili ya kusimamia usalama na kusaidia kuweka vitu sawa kama kutakuwa na changamoto lakini baada ya muda wa majaribio yatakuwa yanasafirisha abiria bila kuwa dereva.
Majaribio hayo yatafanyika kwa muda wa miaka miwili katika majiji, miji na wilaya mbalimbali za nchi hiyo kabla ya kuanza kazi rasmi na kuiongezea Serikali ya nchi hiyo kipato huku ikitarajia kupunguza gharama za uendeshaji.
Majaribio hayo ya kwanza makubwa Barani Ulaya yatafanywa na Kampuni ya Vy kwa kushirikiana na Kampuni ya Kolumbus kwa kutumia teknolojia ya AI (Artificial Intelligence) na sensa kutoka Kampuni ya Adastec na teknolojia ya ufuatiliaji (monitoring technology) kutoka Kampuni ya Norway ya Applied Autonomy.
0 comments:
Post a Comment