Sunday 16 January 2022

WASIOMWAMINI MUNGU WATOA ONYO KANISA LA PEFA KUWAPIGIA KELELE

...
Chama cha Wasioamini Uwepo wa Mungu Kenya (AIK) kimetishia kulishtaki Kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (PEFA), Nairobi kwa kile kilitaja kama uchafuzi wa kelele.

Chama hicho kimesema kimekuwa kikipokea malalamishi kuwa Kanisa la PEFA mtaani Saika hupiga kelele nyingi wakati wa kesha Ijumaa na siku ya Jumapili. Katika barua iliyoandikwa Jumamosi, Januari 15, rais wa chama hicho, Harrison Mumia aliipa kanisa hilo makataa ya siku 14 kupunguza kelele ama lichukuliwe hatua za kisheria.

"Kelele kutoka kwa kanisa la PEFA haiwezi kuvumilika kwa wakazi wengi wanaoishi karibu nalo," ilisoma barua iliyotumwa kwa Askofu John Okinda na Mchungaji Alex Wanyonyi.

Mumia aliongeza kuwa malalamishi hayo si ya wanachama wa AIK bali Wananchi Wakenya ambao wanahisi kanisa hilo linawaharibia starehe zao. 

Waandikia NEMA barua 

Awali, chama hicho kiliandikia Mamlaka ya Kuhifadhi Mazingira (NEMA), barua kikiitaka ifunge maabudu yenye kelele.

Mumia alisema maabudu hayo yanakiuka sheria zilizowekwa za kuzuia uchafuzi wa kelele. 

Kulingana na taarifa iliyotolea siku ya Jumanne, Januari 19, 2021, wasiomwamini Mungu walisema walipokea malalamishi kutoka kwa Wakenya wakidai makanisa hayo yaliwakosesha amani. 

Kwa mfano, Mumia alisema kuna misikiti ambayo huendesha ibada zao kila baada ya saa tano huku wakiwekwa vipasa sauti nje ya majengo yao. 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger