




















(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu amekabidhi zawadi ya washindi wa Mashindano ya Kuimba Chuo kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Yakubu ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kuendeleza na kukuza vipaji vya muziki kwa vijana wa Chuo hicho kwa kuwapatia fursa kuoneshesha vipaji vyao na kuvikuza.
Amesema matamasha kama haya matumaini yake yawe endelevu ili kuendelea kuibua fursa kwa vijana kupitia sanaa ya muziki kwani sanaa ni ajira kwasasa.
"Kukuza matamasha kama haya ili kuibua vipaji kwa vijana na pia kuwa sehemu ya kuwa daraja kwa watu ambao wanahitaji kuonesha na kuvikuza vipaji vyao". Amesema Mhe.Yakubu.
Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),Prof.William Anangisye amesema Chuo kiliandaa Tamasha la Muziki la Wanafunzi ambao hushindana na kuibua vipaji
Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika taifa kwakuwa ni kitovu cha Utafiti, ufundishaji na ujifunzaji.
"Wahitimu wengi wameajiriwa Serikalini, katika Sekta binfasi na mashirika ya Kimataifa kutokana na ubora wa wahitimu katika kufikiri, kuchanganua mambo na kutatua changamoto mbalimbali katika vituo vya kazi, jamii na taifa kwa ujumla". Amesema.
Mshindi wa kwanza wa Tamasha hilo amekabidhiwa kitita cha Shilingi Milioni moja za Kitanzania, Mshindi wa Pili akikabidhiwa shilingi Laki saba na mshindi wa Tatu akiondoka na kitita cha Shilingi laki tano.
Mshindi wa kwanza ambaye aliondoka na kitita hicho Moses Selestin, mshindi wa pili ni Rodhey Rutashwotwa na mshindi wa tatu ulienda kwa Calum Aloyce.
0 comments:
Post a Comment