SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania Mkoani Tanga (TASAC) limetoa wito kwa vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi zake majini ambayo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora kutokwenda majini kufanya shughuli zake.
Agizo hilo lilitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema kwamba wao wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda majini.
Afisa Mfawidhi huyo alisema pia kwa kipindi hicho vyombo vyote vilivyopata vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.
Aidha alisema kwa vyombo ambavyo na vyombo havitakuwa na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini wanavitaka visienda kufanya shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.
“Tunatoa rai kwa vyombo vizingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito”Alisema
Alisema kwamba hivyo kama uwezo wa kutoa maji kwenye chombo utakuwa ni mdogo itakuwa rahisi kuzama na hivyo tunatoa wito kwa vyombo vyote hasa kwa uvuvi maelekezo hayo yazingatiwe.
Hata hivyo aliwataka watendaji wa serikali za vijiji na mitaa maeneo ya vyombo vya uvuvi,mizigo vinapotoka kwenye maeneo yao vimekaguliwa na kupatiwa cheti cha ubora na idadi ya vifaa vya uokozi maalumu baharini kulingana na idadi ya wafanyakazi waliopo kwenye chombo hicho.
0 comments:
Post a Comment