Katika mazungumzo hayo, Bi. Kitomari ameitambulisha MISATAN pamoja na kuelezea majukumu yake mbalimbali kwa Mhe. Jaji Mkuu ikiwemo kutetea na kufanya uzengezi kuhusu utoaji na upataji taarifa nchini.
Mwenyekiti wa MISA amezungumzia uhusiano mzuri uliopo baina ya taasisi yake na Mahakama ya Tanzania ambao umejikita ktk kuimarisha na kutetea haki ya utoaji na upatikanaji wa taarifa zenye maslahi kwa umma.
“Katika hili, MISA kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania tumeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi zaidi ya 300 wa kada mbalimbali za Mahakama kuhusu namna bora ya kuwahudumia wateja na mbinu za utoaji wa taarifa kwaumma” alifafanua Bi. Kitomari.
Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na MISA Tanzania, mafunzo haya yameongeza weledi kwa washiriki na kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa taarifa za Mahakama hapa nchini.
Aidha, Mwenyekiti wa MISA alisisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizi mbili pamoja na kuhusisha taasisi nyingine za kihabari ili kupanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa za kimahakama zenye maslahi ya umma. Bi. Kitomari ameshauri kufanyika mikutano kati ya MISA TAN, Mahakama ya Tanzania na taasisi nyingine za Habari ili kuimarisha ushirikiano, imani na uwajibikaji katika mchakato mzima wa utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa wananchi.
Pia, ameshauri kuwepo kwa mafunzo endelevu ya huduma kwa mteja na upatikanaji wa taarifa kwa kuhusisha viongozi wa juu wa Mahakama wakiwemo Majaji, Mahakimu na afisa tawala.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Tanzania ameipa changamoto MISATAN na taasisi nyingine za Habari nchini kuitekeleza ipasavyo Sheria Namba 6 ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2016 katika kudai taarifa zenye maslahi kwa umma na taifa.
“Sheria hii inatoa shurti ya kutoa taarifa zinazotakiwa na umma, hivyo sio Fadhila bali ni amri. Hivyo ni vyema kuangalia ni kwa namna gani tunatumia sheria hii kushurutisha utoaji wa taarifa sahihi kwa wananchi” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.
Aliongeza kwamba ni wajibu wa kila mmoja kutimiza wajibu wake kikamilifu katika kutekeleza sheria hii ipasavyo. “Kwa kufanya hivyo tutakua tumetekeleza takwa la Kikatiba na kisheria” amehimiza Mhe. Jaji Mkuu.
Kwa upande mwingine, Mhe. Prof. Juma amevitaka vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika kuhabarisha umma ili kuepusha mifarakano katika Jamii.
Amewahimiza waandishi wa habari nchini kujikita zaidi katika kuandika habari za kiuchunguzi badala ya kutegemea habari za matukio.
“Habari za kiuchunguzi huhusisha utafiti na ushahidi wa jambo. Kuripoti habari hizi kutapunguza malalamiko na mifarakano katika jamii” amehitimisha Mhe. Jaji Mkuu.

0 comments:
Post a Comment