Wednesday 1 June 2016

Waziri Mkuu: Serikali Itahakikisha Inaendelea Kulinda Rasilimali Za Nchi Ikiwemo Urithi Wa Dunia

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
SERIKALI ya awamu ya tano  imesema kuwa itaendeleza jitihada za kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana rasilimali za nchi .

Hayo yalisemwa na  waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu unaoendelea jijini Arusha

Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha  inatunza na kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na  kusaidia vizazi vijavyo.

Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira unaotokea kwenye hifadhi za taifa .
 
“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu  kwani hata hizo mali asili zinatusaidia sote na ndiyo sababu  tumewekea mikakati ya kutunza maeneo hayo ili yawe endelevu" alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia  na kuathiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .

Aidha mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.

Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo ya urithi wa dunia  kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.

Mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia utakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageni watakao huthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mitaji wa kijamii” alisema Malinzi

Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger