Thursday 30 June 2016

MPYA:MKURUGENZI WA TBS ATUMBULIWA JIPU,PIA MENEJA WA FEDHA APIGWA CHINI

...

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage leo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa shirika la Viwango Tanzania TBS Bwana Joseph B. Masikitiko ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Pia Waziri Mwijage ameagiza Bwana Emmanuel M. Ntelya Meneja wa Fedha, Mipango na Utawala wa TBS, asimamishwe kazi mara moja kwa kipindi chote ambacho uchunguzi utakuwa unaendelea. Aidha waziri amemteua Dkt Egid B. Mubofu, Mkuu wa Idara ya Kemia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania.

index.jpeg
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger