Monday 20 June 2016

Wabunge kukatwa asilimia 30 ya Sh200 milioni

...

Wabunge wanatarajiwa kukatwa asilimia 30 ya kiinua mgongo chao ambacho kimeelezwa kuwa ni Sh200 milioni. Taarifa zilizopatikana kutoka kwenye Kamati ya Bajeti iliyopitia muswada huo, zimeeleza kuwa asilimia hiyo  inatokana na marekebisho yaliyofanywa na kupitishwa na wabunge wenyewe kwenye Sheria ya Mapato ya 2010. “Marekebisho ya asilimia 30 yalifanyika 2010 lakini huu muswada wa sasa unafuta msamaha hivyo, wabunge watakatwa kodi ya asilimia hiyo ambayo ni sawa na Sh60 milioni kila mmoja,” kimeeleza chanzo chetu. Alipoulizwa kuhusu makato hayo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema  anayeweza kuzungumzia mambo ya Kamati ya Bajeti ni mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia. Hata hivyo, Ghasia alipoombwa kutoa ufafanuzi huo, ameeleza kuwa kamati yake bado inaendelea na kazi






Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger