Saturday 25 June 2016

Joh Makini alia na wahalifu wa mitandaoni

...

Joh-makini.jpgStori:
MKALI katika gemu la Muziki wa Hip Hop, Bongo, John Saimoni ‘Joh Makini’ amefunguka kuwa serikali inatakiwa kuhakikisha inaweka mkazo katika sheria yake inayowataka watu wasifanye uhalifu wa aina yoyote mtandaoni hasa wale wanaotumia elimu yao ya masuala ya mtandao kuwanyanyasa wengine kwa ‘kuhaki’ akaunti zao za mitandao ya kijamii kisha kuzitumia wanavyotaka wao.
Akichonga na gazeti hili Joh alisema amekumbana na kisanga cha kuchukuliwa akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram hivi karibuni jambo lililompa usumbufu wa kuhakikisha anairudisha tena akaunti hiyo mikononi mwake ambayo kwake ni ofisi kwa sababu ni sehemu anayokutana na mashabiki wake kwa urahisi.
“Serikali inatakiwa kuliangalia suala hili kwa mkazo zaidi kwa sababu bado uhalifu wa mitandao unasumbua watu wengi na unasababisha mpaka wengine wanapoteza pesa bila sababu yoyote. Hivi karibuni nilichukuliwa akaunti yangu na imenilazimu kupambana kuirudisha kiasi kwamba nimebadilisha mpaka jina,” alisema. John Makini.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger