Tuesday 25 February 2014

USTADH ALIVYOMCHINJA MTOTO

...

USTADH ALIVYOMCHINJA MTOTO

Stori: Waandishi Wetu
KUFUATIA tukio la Ustadh Mohamed Said Ngulangwa (36), mkazi wa Mbagala-Charambe jijini Dar kumchinja mtoto Jamal Salum Ally (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano kisha na yeye kuuawa na wananchi wenye hasira, Uwazi kama kawaida yake lilichimba tukio hilo na kubaini mengi, twende pamoja.
Mtoto Jamal Salum Ally (12) enzi za uhai wake.
MTOTO AITWA, AENDA
Akizungumza na Uwazi Jumamosi iliyopita msibani Mbagala juzi, mtoto mmoja (jina lipo) alisema yeye na marehemu walikuwa wakicheza michezo ya kawaida, mara akatokea ustadh na kumwita mtoto Jamal.
Ustadh Mohamed Said Ngulangwa (36) enzi za uhai wake.
“Sisi tulikuwa tunacheza, ghafla ustadh akamwita Jamal. We Jamal, njoo. Kwa vile aliita kwa sauti ya kawaida tulijua anataka kumtuma, Jamal akaenda mimi nikawa namsubiria ili tuendelee kucheza, kumbe mwenzangu aliitwa kuchinjwa,” alisema mtoto huyo kwa sura iliyojaa simanzi.
Waombolezaji wakiwa msibani.
KISU KIKALI CHATUMIKA
Mtoto huyo aliendelea kueleza kwa uchungu kwamba, akiwa anamshuhudia Jamal akikutana na ustadh, alishangaa kumwona mwanaume huyo akimdaka kwa haraka na kisha kutoa kisu ambapo alianza kumchomachoma nacho na hatimaye kumlaza chini na kukipitisha shingoni kama anachinja kuku.
Mwili wa ustadh baada ya kuuawa na wananchi wenye hasira kali.
“Nilipiga kelele kuwaambia watu, nikatoka kwenda kuwaita watu huku napiga kelele kwamba Jamal anachinjwa na ustadh,” alisema mtoto huyo huku akionesha sura halisi ya masikitiko ya ndani ya moyo. Inauma sana!
Mwili wa mtoto Jamal baada ya kuchinjwa na ustadh.
MAJIRANI WADHANI ADHABU INATOLEWA
Nao majirani na madrasa ya mtu huyo waliopata nafasi ya kueleza walichojua kuhusu mauaji ya mtoto huyo, walisema kelele za mtoto Jamal kuomba msaada zilisikika, lakini waliamini mtoto anapewa adhabu na mzazi wake.
MAMA WA MAREHEMU AFIKA MBIO
Maelezo zaidi yanasema kuwa, mtoto aliyekwenda kuita watu alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu na kumkuta mama mzazi ambaye alimpa taarifa.
Eneo alilochinjiwa mtoto Jamal.
Mwanamke huyo aliyepewa taarifa hizo, akiwa haamini masikio yake, alitoka mbio na kilio kuelekea eneo la tukio.
Wananchi nao baada ya kusikia maelezo ya mtoto aliyeshuhudia, waligutuka na kutua eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikutana na kichwa kikiwa miguuni mwa kiwiliwili. Lazima umwage machozi!
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
MBALI NA KIWILIWILI NA KICHWA
Wananchi hao waliweza kugundua kuwa, kichwa hicho ni cha mtoto Jamal huku pembeni yake kukiwa na ndoo ambayo walidai muuaji alikusudia kukingia damu (ili iweje?).
VILIO VYATAWALA, USTADH AJIFICHA
Vilio vilianza kutalawa eneo hilo, akina mama, marafiki wa marehemu waliangua vilio vya uchungu baada ya kuuona ukatili huo ambao walisema haujawahi kutokea katika eneo hilo.
Jeneza lenye mwili wa Jamal likiwa mbele ya waombolezaji.
Ilidaiwa kwamba, wakati huo ustadh alikuwa amejificha chumbani kwake ili kuepuka ‘soo’ lake lakini wananchi walishtukia janja yake na kutishia kuvunja dirisha ambapo mtuhumiwa huyo alichungulia akiwa na kisu mkononi kikiwa na mabaki ya damudamu.
WANANCHI WAVUNJA MLANGO, DIRISHA LA USTADH
Bila kujali kisu hicho, wananchi walivunja mlango na dirisha na kuanza kumshambulia kwa mawe, kisha wakamchomoa akiwa uchi wa mnyama mpaka nje huku wakiendelea kumshambulia hadi akakata roho.
Magari ya polisi yakiwa eneo la tukio.
BABA WA MAREHEMU NAYE ANALO NENO LA KUSIKITISHA
Naye baba wa Jamal, Salum Ally alipoongea na Uwazi alitoa simulizi ya majonzi, msikie: “Nilipokea kifo cha mwanangu Jamal kwa huzuni kubwa sana, sikuamini kama yeye ndiye aliyeuawa kikatili namna ile!
“Nilikuwa narudi nyumbani kutoka kazini, jirani na nyumbani nikakuta watu wengi, nikahoji kulikoni? Nikaambiwa kuna mtoto amechinjwa na aliyemchinja ameuawa. Khaa! Nikashangaa!
Baadhi ya watoto waliofika eneo la tukio kushuhudia mwenzao aliyechinjwa.
“Kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana, niliona nifike kwangu kwanza ndipo nirudi kwenye tukio. Kabla ya kutua kwangu, nikakutana na mke wangu njiani huku akilia, nilipomhoji kuna nini, aliendelea kulia bila kunipa majibu.
“Ndipo mpangaji mwenzangu akanipasulia kwa kuniambia kwamba mwanangu Jamal amechinjwa mpaka kichwa kutenganishwa na kiwiliwili.
“Nilipatwa na mshtuko mkubwa kwani sikufikiria kama kungetokea tukio la kutisha kama hilo, hata kama mngekuwa ninyi waandishi mngefanyaje jamani?
Mwili wa Jamal ukiombewa kabla ya maziko.
“Nilijivuta hadi eneo la tukio na kukuta mwili wa mwanangu umeshafungwa kwenye nguo na kuwekwa ndani ya gari la polisi, sikuwa na nguvu ya kuangalia sura yake kwa uchungu nilioupata kwani ndiyo mtoto wa kwanza,” alisema Salum.
USTADAH ALIPANGA MAUAJI?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, ustadh huyo alijiandaa kutekeleza mauaji hayo kwa vile aliandaa kisu na ndoo kwa ajili ya kukingia damu ya mtoto huyo kwa kile watu walichodai alitaka kuinywa.
POLISI MZIGONI
Baadaye taarifa zilienea maeneo yote ya Jiji la Dar hususan Mbagala-Charambe na polisi walitua eneo hilo na kuchukua miili ya marehemu wote wawili na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Temeke.
Mwili wa Jamal ukipelekwa eneo la makaburini kwa maziko.
Pale hospitalini, madaktari walitumia saa mbili kichwa cha mtoto Jamal na kiwiliwili.
USTADH ATAJWA KUTOKUWA NA AKILI
Mdogo wa Ustadh Mohamed aliyekuwa msemaji wa familia, Daudi Ngulangwa alisema marehemu kaka yake aliwahi kupatwa na ugonjwa wa akili mwaka 1995/96 kisha kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutibiwa na akapona.
Maziko ya mtoto Jamal yakifanyika.
MAZISHI YAO
Marehemu Jamal alizikwa Jumamosi iliyopita katika Makaburi ya Mbagala-Charambe jijini Dar (Uwazi lilikuwepo).
Ustadh Mohamed, yeye alizikwa siku hiyohiyo kwenye Makaburi ya Manzese jijini Dar es Salaam.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger