KIGOGO WA CCM...
Na The blogger-boy , SUA
HALI inatisha! Vyama vya Chadema na CCM vinaonekana kuwa chanzo cha baadhi ya watu kubaki na ngeu baada ya juzikati vurugu kutokea katika Kata ya Ubagwe, wilayani Kahama na kusababisha majeraha kwa viongozi na watu mbalimbali.
Vurugu hizo zilitokea Februari 4, mwaka huu, majira ya saa 1:30 usiku kwenye kampeni za CCM zilizokuwa zikifanyika katika Kata ya Ubagwe ambapo Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Alphonce Kimaro alidaiwa kutobolewa jicho la kulia na kujeruhiwa kwenye paji la uso.
Majeruhi mwingine ni Katibu wa UVCCM Kata ya Majengo, Sebastian Masonga, ambaye alisimulia jinsi alivyovunjika mkono na kudai kuwa, siku ya tukio walikuwa wakitokea kwenye mkutano wa kampeni za udiwani, njiani wakavamiwa na vijana waliowashambulia kwa silaha.
“Tulikuwa tukitokea kwenye mkutano wa kampeni, njiani kwenye pori tukakuta magari mawili. Wakashuka vijana wakatuzingira, mmoja wao akavunja mlango kwa shoka na baadhi wakaanza kutuvuta kutoka kwenye gari,” alisimulia Masonga ambaye alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza na kuongeza;
“Kuona hali hiyo, nilifungua mlango wa nyuma wa gari letu aina ya Toyota Land Cruiser nikakimbia ili kujikoa, lakini mmoja wao akanidaka, akaanza kunishambulia kwa nondo.
“Nilipojaribu kukinga mkono nondo ikatua hapo na kunivunja vibaya, alinisachi na akafanikiwa kuchukua kila kitu zikiwemo fedha.”
Kutokana na hali hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ambaye aliwatembelea majeruhi hao, amelaani vikali vurugu hizo alizodai zimefanywa na baadhi ya viongozi wa Chadema wilayani Kahama na kusema madaraka hayawezi kupatikana kwa kumwaga damu.

0 comments:
Post a Comment