TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KWA DHARURA
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa ajili ya kikao cha dharura, Februari
14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu itajadili na
kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea ubunge wa CHADEMA katika
uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, unaotarajiwa
kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Kikao hicho kitafanya uteuzi wa mwisho,
baada ya mchakato wa ndani wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga
kwa tiketi ya CHADEMA, kuwa umepitia hatua za awali, ambazo ni…
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KWA DHARURA
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa ajili ya kikao cha dharura, Februari
14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu itajadili na
kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea ubunge wa CHADEMA katika
uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, unaotarajiwa
kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Kikao hicho kitafanya uteuzi wa mwisho,
baada ya mchakato wa ndani wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga
kwa tiketi ya CHADEMA, kuwa umepitia hatua za awali, ambazo ni pamoja
na watu wote wenye nia ya kugombea, kuchukua fomu za uteuzi, tangu
Februari 5-10, mwaka huu.
Kama ilivyoelezwa kwa umma kupitia vyombo
vya habari, Februari 6, mwaka huu, fomu hizo zilitolewa katika maeneo
matatu, Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, Ofisi za Jimbo la
Kalenga na kwenye tovuti ya chama, ambayo ni; www.chadema.or.tz.
Jumla ya watu 16 waliweza kuchukua fomu za
kuwania uteuzi huo, ambapo hadi siku ya mwisho, watu 13 waliweza
kurejesha fomu zao na kupita kwenye mchakato wa kura za maoni,
zilizofanyika Februari 12, mwaka huu.
Imetolewa leo Februari 13, 2014, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
0 comments:
Post a Comment