Monday, 3 October 2022

MASHIRIKA YANAYO LEA USHOGA YAONYWA

...


Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza.

Na Dotto Kwilasa,DODOMA


MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza, ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yatajihusisha na kutetea ndoa za jinsia moja  kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za kitanzania.


Mahiza, amezungumza hayo  jijini Dodoma, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali na kueleza kuwa yapo mashirika  nchini yanaishi kwa kivuli Cha kutetea ushoga kwa madai ya kulinda haki za binadamu.


Amesema, katika kipindi chake akiwa mwenyekiti wa Bodi hiyo hatopenda kuona jambo hilo linatokea kwa kuwa ni kinyume na mila na desturi za Watanzania na ni aibu .


“Kama kuna shirika lolote ambalo katika utekelezaji wa majukumu yake limepanga kufanya vitu kama hivyo naomba lifute mpango huo mara moja hatuwezi kuviruhusu vitu kama hivi katika taifa ambalo serikali ipo na dini zipo”amesema Mwantumu na kuongeza;

Si jambo la busara kwa taifa kuruhusu vitendo vya ndoa za jinsia moja kwa mwanamke kuolewa na mwanamke mwezake au mwaume kuoa mwanaume mwenzake , tusipofanya juhudi tutashindwa kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke,"anasisitiza 


Pamoja na hayo ametilia mkazo suala hilo kuwa Serikali  haiwezi kuruhu haki za binadamu zinazopingana na mila na kueleza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake ni kubwa ukilinganisha na wanaume hivyo ndoa za jinsia moja ni jambo ambalo halipaswi kupewa nafasi.


“Hata ukienda leo hospitali kati ya watoto kumi wanaozaliwa kwa siku wanawake ni saba wanaume ni watatu hivyo kama tusipokuwa makini hii nchi itakuwa ya wanawake tupu wanaume watakwisha kwasababu wanaoana wao kwa wao”amesisitiza


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema lengo la mkutano huo ni pamoja kupata fursa ya kukumbushana mambo mbalimbali.


Mkurugenzi huyo pia ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali kufanyia marekebisho ya sera inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni pamoja na kuyaondolea kodi katika vitu mbalimbali ambavyo wamekuwa wakiingiza kutoka nje ya nchi.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger